Faida za Kuwa Mwanachama wa USHIRA
Jiunge na jamii inayothamini nidhamu, uwazi, mshikamano na maendeleo ya pamoja. Hapa, huna tena sababu ya kupitia changamoto au kufurahia mafanikio peke yako.
Kwa nini Uchague USHIRA?
Tunatoa zaidi ya mfumo wa kifedha — tunatoa jamii, ulinzi, nidhamu na maendeleo ya kweli.
Ulinzi wa Kifedha
Mwanachama hupata mfumo wa kusaidiana wakati wa changamoto za kifedha na dharura za kimaisha. Hukabiliani na shida peke yako — usaidizi unakuja kwako kwa wakati.
M-Koba Mix
Mfumo maalum wa kuweka na kukuza fedha kwa usalama, kwa misingi ya nidhamu ya kifedha na mshikamano, unaokusaidia kufikia malengo yako ya akiba na ukuaji.
Bima ya Maisha
USHIRA inalenga kuwajali wanachama na familia zao kupitia mifumo ya kinga na usaidizi wa maisha. Familia yako haibaki nyuma — tunakuhakikishia ulinzi.
Bima ya Afya
Wanachama wanaelekezwa na kusaidiwa kupata huduma za afya na mipango ya kinga ya afya. Afya yako ni muhimu kwetu, tunakusaidia kupata huduma bora.
Elimu ya Biashara
Wanachama hupata mafunzo, elimu ya biashara, ujasiriamali, mindset ya maendeleo na mbinu za kujiongezea kipato. Tunakujenga kiakili na kiuchumi.
Msaada Tutani
Msaada Tutani ni mfumo wa msaada wa kifedha kwa wanachama hai wa USHIRA ambapo mwanachama anaweza kupata mkopo wa riba nafuu au kusaidiwa fedha ya muda pale anapokwama. Mwanachama anaweza kusaidiwa kutuma mchango wa siku kwenye ‘Sisi kwa Sisi’ anapopata changamoto ya muda mfupi. Marejesho yanafanywa kidogo kidogo kwa urahisi mkubwa. Mfumo umejengwa kwa matumaini, mshikamano na kuinuana.
Mtandao wa Fursa
USHIRA huunganisha watu wenye malengo, biashara, kazi na fursa mbalimbali za maendeleo. Mtandao wako unapanuka na fursa mpya zinazidi kukujia.
Ukuaji wa Nidhamu ya Fedha
Unajifunza saving culture, consistency na financial discipline. Mfumo unakufundisha jinsi ya kusimamia fedha zako kwa busara na kujenga mustakabali imara kiuchumi.
Mfumo wa Umoja na Uaminifu
USHIRA imejengwa juu ya misingi thabiti ya uwajibikaji, uwazi na ushirikiano. Kila mwanachama anafuatiliwa kwa mfumo wa kidigitali unaohakikisha usalama wa taarifa na kujenga jamii yenye kusaidiana kwa heshima na uaminifu.
Jinsi ya Kujiunga
Hatua tatu tu, na unakuwa sehemu ya familia yetu inayokua kwa nidhamu na mshikamano
Jaza Taarifa Zako
Kamilisha fomu ya usajili kwa taarifa zako sahihi na halisi kwa usalama na uthibitisho kamili wa KYC.
Jiunge Rasmi kwenye Mfumo
Baada ya uthibitisho, unakuwa mshiriki na kuanza kufurahia huduma za mfumo wetu kikamilifu.
Anza Kufurahia Faida
Ukiwa mwanachama, unapata ulinzi, nafasi za kujifunza, mtandao, na fursa mbalimbali za kukua na maendeleo.
Wanachama Wanasema
Hatimid za wanachama waliojiunga na kujionea mabadiliko katika maisha yao
Mariam Juma
Mwanachama, Dar es Salaam
James Mwita
Mfanyabiashara, Mwanza
Uko Tayari Kuwa Mwanachama?
Jiunge na jamii ya watu wenye malengo, wanaothamini nidhamu, uwajibikaji na mshikamano wa kweli. Pamoja tunaweza kufikia zaidi.