Sisi kwa Sisi Tuinuane - Umoja wa Shida na Raha
MFUMO WA KINIDHAMU NA USHIRIKIANO

Sisi kwa Sisi Tuinuane

"Kila Siku Tunajenga, Kila Siku Tunainuka"

Mpango wa hiari wa kijamii wa mzunguko wa michango ya kila siku (upatu wa kidijitali) unaoendeshwa kupitia magroup ya WhatsApp kwa mpangilio rasmi na uwazi. Si mkopo, si uwekezaji, na hauna dhamana ya faida.

UELEWA MFUMO

Sisi kwa Sisi ni nini?

Mpango wa hiari wa kijamii wa mzunguko wa michango ya kila siku unaoendeshwa kidigitali kwa ushirikiano wa wanachama wenye nidhamu na uwajibikaji.

Mzunguko wa Michango ya Kila Siku

Sisi kwa Sisi Tuinuane ni mpango wa hiari wa kijamii wa mzunguko wa michango ya kila siku (upatu wa kidijitali) unaoendeshwa kupitia magroup ya WhatsApp na Msimamizi Mkuu, chini ya Sehemu ya Kumi ya Katiba ya Umoja wa Shida na Raha. Kila kundi lina nafasi 100 na hudumu kwa siku 100. Kila siku mshiriki mmoja hupokea mchango wa siku hiyo baada ya kukusanywa, siku hiyo hiyo.

Mpango si mkopo, si uwekezaji, si benki wala si dhamana ya faida. Hakuna anayeahidiwa kipato zaidi ya kiasi cha zamu yake kilichoainishwa. Michango ya kila siku inatumwa kwenye namba rasmi 0759310090 (RIZIKIEL ADAM MMARI) pekee, kabla ya saa 2:00 usiku kila siku.

VIWANGO VYA MZUNGUKO

Chagua Kiwango Kinachokufaa

Kuna viwango vitano tofauti kulingana na uwezo wako na malengo yako

Starter

Changia: TSh 1,100 kwa siku
Makato: TSh 100 kwa jina
Unapokea: TSh 100,000 (nafasi 1)

Basic

Changia: TSh 2,200 kwa siku
Makato: TSh 200 kwa jina
Unapokea: TSh 200,000 (nafasi 1)

Silver

Changia: TSh 5,500 kwa siku
Makato: TSh 500 kwa jina
Unapokea: TSh 500,000 (nafasi 1)

Gold

Changia: TSh 11,000 kwa siku
Makato: TSh 1,000 kwa jina
Unapokea: TSh 1,000,000 (nafasi 1)

Diamond

Changia: TSh 22,000 kwa siku
Makato: TSh 2,000 kwa jina
Unapokea: TSh 2,000,000 (nafasi 1)

MCHAKATO RAHISI

Jinsi Mfumo Unavyofanya Kazi

Hatua nne rahisi za kuanza safari yako ya ukuaji wa kifedha kwa mshikamano

1

Jisajili na Chagua Kiwango

Jaza fomu ya usajili kwa taarifa zako sahihi (jina kamili kama kwenye NIDA, namba ya NIDA, simu, anwani na Next of Kin) na chagua kiwango cha mzunguko.

2

Uhakiki wa Taarifa (KYC)

Taarifa zako zitathibitishwa kuhakikisha usalama, uaminifu na uwajibikaji ndani ya mfumo. Ridhaa inathibitishwa kwa kutia tiki kwenye fomu ya kujisajili.

3

Ingia Kwenye Mzunguko

Utaingizwa kwenye kundi la WhatsApp la wanachama wa kiwango chako. Ratiba rasmi ya zamu itatolewa kabla ya mzunguko kuanza.

4

Changia na Pokea Zamu

Kila siku unachangia kiasi chako kabla ya saa 2:00 usiku. Siku yako ikifika, unapokea kiasi cha daraja lako baada ya makato na faini yoyote.

FAIDA ZA MFUMO

Kwa nini Ushiriki Sisi kwa Sisi?

Manufaa ya kuwa sehemu ya mfumo wetu wenye nidhamu na uwazi

Nidhamu ya Fedha

Mfumo unakusaidia kujenga utamaduni wa mpangilio wa matumizi na akiba ya kila siku, na kukufundisha uwajibikaji wa kifedha.

Mtandao wa Watu Wenye Malengo

Unajiunga na jamii ya watu wanaofuata kanuni sawa za nidhamu na kujituma kufikia malengo yao ya kiuchumi.

Uwazi Kamili wa Kidigitali

Kila mchango na malipo yanafanyika moja kwa moja kati ya wanachama kwa uwazi unaoonekana na wote kupitia Mkea (ripoti ya michango na zamu).

Uwajibikaji wa Kila Siku

Ushiriki wa kila siku unakuweka katika mfumo unaokufanya uweze kupimika na kuwajibika katika kila hatua.

KUELEWA MFUMO

Tofauti ya Mshiriki na Mwanachama

Kuelewa tofauti kati ya ushiriki wa Sisi kwa Sisi na uanachama kamili wa Umoja wa Shida na Raha

Mshiriki wa Sisi kwa Sisi

Anayeshiriki Mzunguko wa Kifedha

  • Anachangia kila siku kwa mzunguko
  • Anapokea pesa kwa zamu iliyopangwa
  • Lengo kuu ni kuinuka kiuchumi kwa pamoja
  • Ushiriki huu peke yake haukumfanyi uwe mwanachama wa Umoja wa Shida na Raha
Mwanachama wa Umoja wa Shida na Raha

Mwanachama Hai wa Umoja

  • Amelipa kiingilio cha TSh 50,000 (mara moja)
  • Amekamilisha uhakiki wa taarifa (KYC)
  • Amelipa mchango wa welfare wa TSh 20,000 kwa mwezi
  • Ameridhia Katiba na Kanuni za Umoja
  • Kupata haki ya Pole, Pongezi na Bima

Muhimu Kuelewa

✓ Unaweza kuwa mshiriki wa "Sisi kwa Sisi" bila kuwa mwanachama wa Umoja wa Shida na Raha.
✗ Lakini huwezi kabisa kuwa mwanachama wa Umoja wa Shida na Raha bila kuwa mshiriki wa "Sisi kwa Sisi" na kupitia uthibitisho kamili wa KYC.
Sisi kwa Sisi ni lango; Umoja wa Shida na Raha ndio mfumo mzima wa kijamii na kiuchumi.

UWAZI NA NIDHAMU

Mfumo wa Uwajibikaji wa Kidigitali

Mfumo unaojengwa juu ya uwazi, ufuatiliaji na uwajibikaji wa pamoja

Mawasiliano ya Kila Siku

Kila kundi la Sisi kwa Sisi lina kikundi cha WhatsApp kinachoratibiwa na kusimamiwa kwa nidhamu kali na utaratibu maalum.

Mkea na Rekodi za Uwajibikaji

Mkea ni ripoti ya michango na zamu inayoboreshwa kwenye Google Sheets na kutolewa kwenye group. Rekodi za michango, malipo, faini na makato huhifadhiwa kwa muda usiopungua miaka mitano (5).

Ufuatiliaji wa Nidhamu

Mfumo unaowezesha kutambua wanachama wenye nidhamu wanaofaa kupanda hatua na kuwa sehemu ya mfumo wa kudumu.

SHERIA MUHIMU

Masharti ya Muhimu ya Kufuata

Kila mshiriki anapaswa kuyafahamu na kuyakubali masharti haya

Muda wa Malipo

Michango yote ya kila siku inapaswa kulipwa kabla ya saa 2:00 usiku kila siku (saa za Afrika Mashariki).

Faini ya Kuchelewa

Kuchelewa kunatozwa faini kwa siku kwa kila nafasi. Mfano: daraja la 2,200 lina faini ya TSh 2,000 kwa siku. Kimya bila taarifa huhesabiwa kuwa kuchelewa.

Kujitoa

Siku 2 bila kulipa na bila taarifa ni kujitoa. Hakuna marejesho ya michango iliyokwisha kutolewa; nafasi yako inaweza kupewa mshiriki mwingine kwa idhini ya Msimamizi.

Baada ya Kupokea Zamu

Ukishapokea zamu yako, bado unawajibika kumaliza michango yote iliyosalia. Ukiacha, unabaki na deni na hatua za ufuatiliaji zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni.

MALIPO RASMI

Namba ya Malipo

Malipo yote ya Mpango wa Sisi kwa Sisi yanatumwa kwenye namba rasmi pekee

0759310090 (RIZIKIEL ADAM MMARI)

Michango yote ya kila siku ya Mpango wa Sisi kwa Sisi inatumwa kwenye namba hii pekee. Usitume pesa kwa namba nyingine yoyote. Malipo nje ya namba hii hayatambuliki, na Mpango haubebi dhima ya malipo yaliyotumwa kwa mtu mwingine.

Kiingilio (TSh 50,000) na welfare (TSh 20,000 kwa mwezi) havilipwi kwenye namba hii, bali kwenye Lipa Namba au akaunti ya Umoja wa Shida na Raha itakayotangazwa rasmi.

WALIOFAIKIWA

Nani Anafanikiwa Ndani ya Mfumo?

Watu wenye sifa maalum ndio wanaoendelea kufaulu ndani ya mfumo wetu

Wenye Nidhamu ya Fedha

Wanaojua umuhimu wa mpangilio wa matumizi na akiba, na wako tayari kujenga tabia ya kifedha inayowafaa.

Wanaoheshimu Makubaliano

Wanaotambua kuwa ahadi zetu ndani ya mfumo ni mtakatifu kwa ustawi wa wote wanaotegemea mfumo huu.

Wanajenga kwa Muda Mrefu

Wanaotaka kujenga misingi imara kwa maisha yao na familia zao, si wanaotafuta faida za haraka.

Huu SI mfumo wa:

Kukimbilia kupata pesa haraka • Kujaribu bahati nasibu • Kukwepa uwajibikaji • Kutafuta njia ya mkato ya utajiri

Uko Tayari Kuanza Safari Yako?

Si kila mtu anafaa kuwa sehemu ya mfumo huu. Lakini kama wewe una nidhamu, malengo, na uko tayari kujenga maisha kwa misingi imara — tunakukaribisha kwa mikono miwili.