Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara - USHIRA
MASWALI MARA KWA MARA

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Pata ufafanuzi wa kina kuhusu USHIRA na mfumo wa Sisi kwa Sisi Tuinuane.

Uwazi Nidhamu Ushirikiano
USHIRA ni nini?

USHIRA (Umoja wa Shida na Raha) ni mfumo wa kijamii na kiuchumi unaowaunganisha watu wenye malengo kupitia uwajibikaji, nidhamu ya fedha na mshikamano wa kweli. Sio benki, sio kampuni ya mkopo, na sio jukwaa la uwekezaji.

Lengo kuu la USHIRA ni nini?

Kujenga jamii yenye watu wanaosaidiana katika shida na raha huku wakijenga uthabiti wa kifedha na kijamii kwa pamoja. USHIRA inalenga kuondoa hali ya mtu kubaki peke yake wakati wa changamoto au mafanikio.

Je, USHIRA ni kampuni?

Hapana. USHIRA ni mfumo wa kijamii wenye kanuni, taratibu na mwongozo wa uendeshaji unaolenga mshikamano na uwajibikaji wa pamoja. Huu ni umoja wa wanachama, sio shirika la kibiashara.

Sisi kwa Sisi Tuinuane ni nini?

Ni mfumo wa mzunguko wa kifedha unaowawezesha washiriki kusaidiana kwa mfumo wa kupokezana kupitia makubaliano ya wazi. Mfumo huu unaendeshwa kidigitali kwa uwazi kamili.

Je, kushiriki Sisi kwa Sisi kunamaanisha nimekuwa mwanachama wa USHIRA?

Hapana. Unaweza kuwa mshiriki wa Sisi kwa Sisi bila kuwa mwanachama rasmi wa USHIRA. Hata hivyo, huwezi kuwa mwanachama wa USHIRA bila kwanza kuwa mshiriki wa Sisi kwa Sisi.

Kwa nini Sisi kwa Sisi ni msingi wa USHIRA?

Kwa sababu mfumo huo unasaidia kujenga nidhamu, uwajibikaji na kutambua mwenendo wa wanachama kupitia ushiriki wa kila siku. Sisi kwa Sisi ndiyo injini, na USHIRA ndiyo mfumo mzima wa kijamii na kiuchumi.

Nani anaruhusiwa kuwa mwanachama?

Mtu mwenye nidhamu ya fedha, anayeheshimu makubaliano na mwenye utayari wa kushiriki kwa uwazi na uwajibikaji. Mwanachama lazima awe na umri usiopungua miaka 20 na awe na akili timamu.

Je, lazima niwe mshiriki wa Sisi kwa Sisi ili kuwa mwanachama wa USHIRA?

Ndiyo. Ushiriki kwenye mfumo wa Sisi kwa Sisi ni moja ya vigezo vya kuthibitisha uanachama. Hii ni hatua ya lazima kwa kila mtu anayetaka kuwa Mwanachama Hai wa USHIRA.

Je, mwanachama anatakiwa kuwa na KYC?

Ndiyo. Mfumo unatambua umuhimu wa uthibitisho wa taarifa kwa usalama na uwazi wa wanachama wote. KYC inasaidia kulinda ubora wa mfumo na kujenga uaminifu.

Michango inafanyikaje?

Michango hufanyika kwa utaratibu wa wazi kupitia mifumo rasmi ya fedha iliyokubaliwa ndani ya group husika. Kila mchango unafanyika moja kwa moja kati ya wanachama kwa uwazi unaoonekana na wote.

Je, kuna viwango tofauti vya ushiriki?

Ndiyo. Mfumo una viwango vitano tofauti: TSh 1,100 (Starter), 2,200 (Basic), 5,500 (Silver), 11,000 (Gold), na 22,000 (Diamond) kwa siku.

Je, nikichelewa kuchangia inakuwaje?

Mfumo unazingatia nidhamu. Kutochelewa ni sehemu ya uwajibikaji wa mwanachama au mshiriki. Kuchelewa kunaweza kusababisha faini kulingana na kanuni za mfumo.

Mfumo una usalama gani?

USHIRA inazingatia uwazi wa taarifa, mawasiliano ya wazi, uthibitisho wa taarifa za washiriki na rekodi za mizunguko. Taarifa zote za wanachama zinalindwa kwa teknolojia ya usimbaji.

Je, miamala inafanyika kwa siri?

Hapana. Mfumo unahimiza uwazi ili kila mshiriki aweze kufuatilia mwenendo wa shughuli kwa urahisi. Kila muamala unaonekana na wanachama wote wa kundi.

Mawasiliano yanafanyika wapi?

Kwa kiasi kikubwa kupitia WhatsApp groups rasmi za mfundo, pamoja na mikutano ya mtandaoni na nyaraka rasmi kupitia tovuti.

Kwa nini WhatsApp groups ni muhimu?

Ndizo zinazoleta ukaribu wa wanachama, taarifa za kila siku, uwazi wa shughuli na urahisi wa mawasiliano. Hapa ndipo mzunguko wa kila siku unapoendeshwa.

Je, kila mshiriki anawekwa kwenye group?

Ndiyo, baada ya kuthibitishwa kulingana na utaratibu wa mfumo. Kila mzunguko una group lake maalum la WhatsApp linalosimamiwa na Sekretarieti.

Kwa nini katiba ni muhimu?

Katiba ndiyo msingi wa uendeshaji wa mfumo na inalinda haki, wajibu na uwajibikaji wa wanachama wote. Ni mwongozo rasmi wa uendeshaji wa USHIRA.

Je, kuna sheria za mfumo?

Ndiyo. Kila mshiriki au mwanachama anatakiwa kuziheshimu na kuzifuata. Mfumo una Kamati ya Maadili na Nidhamu inayoshughulikia ukiukaji wa kanuni.

Nitaanzaje?

Jaza taarifa zako kupitia mfumo rasmi wa usajili kwenye tovuti ya USHIRA na fuata maelekezo utakayopewa kwa hatua za kujiunga.

Nini kinachofuata baada ya usajili?

Utapangiwa utaratibu wa kuunganishwa kwenye mfumo husika na kupata maelekezo rasmi. Sekretarieti itakusaidia kukuelekeza kwenye hatua za kuanza ushiriki wako.

THAMANI ZETU

Misingi ya Uendeshaji wa Mfumo

USHIRA imejengwa juu ya misingi thabiti ya uwazi, nidhamu na ushirikiano wa kweli

Uwazi wa Mfumo

Taarifa zote za kifedha na maamuzi ya uongozi ni wazi na kupatikana kwa wanachama wote wakati wote.

Nidhamu ya Wanachama

Kila mwanachama anafuata sheria na kanuni zilizowekwa kwa ukamilifu bila upendeleo wa aina yoyote.

Ushirikiano wa Kijamii

Tunajenga jamii yenye watu wanaosimama pamoja kwa nguvu moja, wakisaidiana katika shida na furaha.

Bado Una Swali?

Kama unahitaji ufafanuzi zaidi kuhusu mfumo wa USHIRA au Sisi kwa Sisi Tuinuane, unaweza kuwasiliana nasi moja kwa moja.